Karibu Chuo cha ualimu Tarime

  

Chuo cha ualimu Tarime kilifunguliwa mwaka 1974,kikiwa na takribani wanachuo 190 wa daraja la IIIC.Mafunzo  ya ualimu daraja yalifundishwa kwa muda wa miaka miwili miwili (2). Chuo hiki kilifunguliwa katika majengo ya shule  ya msingi ya kati Tarime  (Tarime middle School) yaliyojengwa tangu mwaka 1938.Wanafunzi waliokuwa wakisoma katika shule hii ya Tarime Middle School walihamishiwa shule ya msingi Rebu.

Mafunzo ya Ualimu daraja la IIIC yaliendelea kufundishwa mpaka  mwaka 1982.Baadaye  mafunzo haya ya ualimu daraja la IIIC  yalibadilishwa na kuwa mafunzo ya ualimuu daraja la IIIB yakifundishwa kwa muda wa miaka mitatu mitatu (3).

Mwaka 1938 mafunzo ya ualimu daraja la IIIB yaliongezwa muda wa mafunzo kutoka miaka mitatu (3)kwenda miaka mine (4).Katika mabadiliko hayo ya muda wa mafunzo,mitaala iliyofundishwa ilikuwa miaka miwili ya mwanzo wanachuo walifundishwa taaluma ya kidato cha kwanza na cha pili na miaka miwili ya mwisho walifundishwa taaluma ya ualimu. Sifa za kuingia katika mafunzo ya ualimu daraja la IIIC  na IIIB ni mwanchuo kuwa amehitimu Elimu ya msingi na kufaulu.

Mwaka 1990 chuo kilianza kufundisha mafunzo ya ualimu daraja la IIIA na kufanya chuo kufundisha kozi mbili ya ualimu daraja la IIIA na ualimu daraja la IIIB.Sifa za kuingia mafunzo ya ualimu daraja la IIIA ni ufaulu katika mtihani wa kidato cha Nne(CSEE).

Mwaka 1992 mwezi wa Mei wanachuo waliokua wanasoma kozi ya ualimu daraja la IIIA walihitimu kwa mara ya kwanza.

Mwaka 1996 chuo kilifundisha mafunzo ya ualimu kazini yaloyoitwa C-OLevel kwa ajili ya kuwa fundisha walimu kazini kupata elimu ya sekondari (kidato cha nne). Walimu kazini waliohitimu  C­­­­­­­­-0 level na kufaulu mtihani wa kidato cha nne (CSEE) walichaguliwa kusoma mafunzo ya C-Alevel  na baadaye kufanya mtihani wa ualimu daraja la IIIA na waliofaulu walitunukiwa  Cheti cha ualimu daraja la IIIA.

Chuo cha ualimu Tarime kimefundisha mafunzo ya MUKA mwaka 2006-2007, walimu 1444 walihitimu bmafunzo hayo na yaliendeshwa kwa ushirikiano wa chuo na wizara ya Elimu na Utamaduni.Wahitimu wa mafunzo ya MUKA waliofaulu katika mitihani yao ya mwisho iliyotungwa na Baraza la Mitihani la Tanzania walitunukiwa vyeti vya ualimu Daraja la IIIA.

Chuo kimekuwa kikiendesha mafunzo mbalimbali ya Ualimu ka ma vile mafunzo ya kuimarisha utendaji wa kazi (Capacity building),mafunzo ya uongozi kwa walimu wakuu,yaliyokuwa yakidhaminiwa na mgodi wa Nyamongo (BARRICK0,na kuendesha semina mbalimbali za Mazingira,UKIMWI na ufundishaji.

Mwaka 2010 chuo kilianza kufundisha Mafunzo ya ualimu Daraja la IIIA Mchezo.Kozi hii inafundishwa  kwa miaka miwili sawa na kozi ya Ualimu Elimu ya Msingi.

Majina ya wakuu wa Chuo hiki waliongoza Tangu mwaka 1974 hadi 2011.

 

WAKUU WA VYUO
1.       DR.C.C. MAGOTI
2.       N.KOMBA
3.       J.G.GULASHI
4.       E.H.KAVALMBI
5.       A.L. BINDE
6.       F.N.P.K.RWILOMBA
7.       D.M.NDABISE
8.       L.SAMWELI –KAIMU
9.       M.BALAMPAMA

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *